Swali: Kuhusiana na Udhhiyah. Mtu kisafiri kutoka katika nchi yake kwenda katika njia nyingine. Je, achinje katika nchi ile aliyokwenda au awakilishe mtu amchinjie?

Ibn ´Uthaymiyn: Amesafiri pamoja na familia yake au wamebaki katika nchi yake?

Muulizaji: Wamebaki katika nchi yake.

Ibn ´Uthaymiyn: Wamebaki hawakusafiri?

Muulizaji: Ndio, wamebaki hawakusafiri.

Jibu: Basi lillo bora ni yeye awakilishe mtu ambaye anaweza kuwachinjia familia yake ili familia iweze kufurahika kwa Udhhiyah hiyo.

Swali: Ikiwa amesafiri pamoja na familia yake?

Jibu: Wachinje pale ambapo ´Iyd itawakuta.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ al-Maftuuh (92)
  • Imechapishwa: 18/08/2018