Msafiri amenuia kukata swawm yake


Swali: Kuna mtu amenuia kutofunga katika Ramadhaan ilihali ni msafiri. Halafu baadaye akabadili nia yake na akanuia kuendelea na swawm yake. Je, anahesabika ni mwenye kufunga au swawm yake imeharibika?

Jibu: Akitia nia ya kukata kabisa kwamba hafungi basi asiendelee na swawm yake. Swawm inategemea na nia. Ama ikiwa ametia nia ya kusema kwamba kuna uwezekano nikafungua ikiwa joto litanishinda au manuwizi mfano wa na wakati huohuo akawa hakula, basi anaweza kuendelea na swawm yake. Kinachozingatiwa ni manuwizi yake. Akinuia basi atatakiwa kukata swawm yake. Vinginevyo aendelee na swawm yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (30) http://binothaimeen.net/content/693