Msafiri ameenda katika mji unaotegemea mahesabu ya kinyota

Swali: Je, tufunge tukiwa katika miji ya Kiislamu ambayo inategemea mahesabu ya kinyota wakati wa mwezi mwandamo na hawategemei kuuona mwezi?

Jibu: Mko na khiyari, nyinyi ni wasafiri. Wanachuoni wengi wanaona kuwa bora kwa msafiri ni yeye kutokufunga ijapokuwa hatohisi uzito. Kujengea juu ya maoni haya kuleni na msifunge na pindi mtaporejea katika miji yenu mtatendea kazi kwa muqtadha wa kuthibiti kuingia au kuishi kwa mwezi kwa kuuona mwezi mwandamo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´laam-ul-Musaafiriyn, uk. 76
  • Imechapishwa: 30/05/2019