Swali: Je, inajuzu kuchukua msaada kutoka katika miji ya makafiri ili tuweze kushinda na kuzima maandamano katika miji ya kiarabu?

Jibu: Makafiri hawawatakii mazuri waislamu. Wao wanataka maslahi yao. Wanajichanganya ili wachukue matunda yao wao. Waislamu wataishilia kupigana na kuuana huku wao wanachuma matunda. Hatuwezi katu kuwaamini makafiri. Wala hatuwaingizi katika matatizo yetu na kutatua matatizo yetu.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=d4NPCR1q418
  • Imechapishwa: 06/09/2020