Mpangilio wa ulipaji kwa ambaye amepitwa na swalah nyingi

Swali: Mtu ambaye amelala na kukosa ´Aswr na Maghrib na akaamka muda kidogo kabla ya kuingia ´Ishaa muda ambao haumtoshi isipokuwa kulipa swalah ya faradhi moja atangulize nini?

Jibu: Aswali Dhuhr na ´Aswr kisha aswali Maghrib na ´Ishaa.

Swali: Si atangulize Maghrib ili swalah zilizompita zisizidi kuwa nyingi?

Jibu: Baadhi yao wanasema kuwa muda ukiwa mfinyu basi atangulize ile swalah ya sasa. Lakini udhahiri wa maandiko ni kinyume na hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayelala na kupitikiwa na swalah au akaisahau basi aiswali pale atakapokumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”

Hii ni dalili kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anatakiwa kuanza ile aliyosahau kisha ndio aswali ile ya sasa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21597/ما-ترتيب-القضاء-لمن-نام-عن-عدة-صلوات
  • Imechapishwa: 27/08/2022