Mpaka wa mwanafunzi


Swali: Je, mwanafunzi alinganie katika yale aliyojifunza kwa elimu na yakini au ni lazima atumie kwanza miaka katika kusoma kisha baada ya hapo ndio alinganie katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall)?

Jibu: Alinganie katika kitu ambacho amejifunza na kukijua. Kuhusiana na kitu ambacho hakujifunza na hakijui asikiingilie. Alinganie kwa kiasi cha elimu alionayo na asivuke hapo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14819
  • Imechapishwa: 16/04/2018