35Kama ndugu yako amekuwa maskini hata asiweze kujitunza mwenyewe akiwa pamoja nawe, ni lazima umtunze aendelee kuishi nawe; mtendee kama mgeni au msafiri aliye kwako. 36Usimtake akulipe riba ya namna yoyote ile. Ila mche Mungu, naye ndugu yako apate kuishi pamoja nawe. 37Usimkopeshe fedha kwa riba au kumpa chakula ili akulipe faida. 38Mimi ndiye Mwenyezi Mungu, Mungu wako, niliyekutoa nchini Misri ili kukupa nchi ya Kanaani, na ili nami niwe Mungu wako.

  • Marejeo: Walawi 25:35
  • Imechapishwa: 03/02/2020