Miongoni mwa makosa makubwa na yenye khatari zaidi ni zile fatwa za watu hii leo wenye zinazojuzisha picha. Hawajali kwamba fatwa hizi zinapelekea katika kumuasi Allaah (Ta´ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hayo ni kwa kule kupingana na zile Hadiyth zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zinazokataza aina zote za picha na kufanya makemeo kwa njia yenye kuenea. Kadhalika (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametoa amri ya jumla ya kuziharibu picha zote. Watu hawa hawakujali ya kwamba fatwa hizi ni upotevu unaopelekea kuwapoteza watu. Allaah (Ta´ala) amesema:

لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ

“Ili wabebe mizigo [ya madhambi] yao kamili Siku ya Qiyaamah na mizigo ya wale waliowapoteza bila ya elimu. Tanabahi! Uovu ulioje wanayoyabeba.” (16:25)

Imethibiti kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kupata fatwa bila ya dalili, basi dhambi ziko juu ya yule aliyempa fatwa hiyo.”

Wale wenye kujuzisha picha wanatakiwa kuizingatia Aayah hii na Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) na wala wasijiaminishe ya kwamba hawatokuwa na deni kubwa juu ya wale wanaofuata fatwa zao batili na maono yao yaliyoharibika.

  • Mhusika: ´Allaamah Hamuud bin ´Abdillaah at-Tuwayjiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taghliydhw-ul-Malaam, uk. 65
  • Imechapishwa: 29/07/2017