Mnywaji pombe ni kama mwabudu sanamu

Swali: Ni vipi tutaoanisha maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mlevi ni kama mwabudu sanamu.”[1]

na kile kinachotambulika ya kwamba unywaji pombe haumtoi mtu katika Uislamu?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakusema kuwa kunamtoa mtu katika Uislamu. Alichosema:

“… ni kama mwabudu sanamu.”

Bi maana anafungamana nayo kama ambavyo mwabudu sanamu anavyofungamana na sanamu.

[1] Dogo liwezalo kusemwa ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”an-Naswiyhah”, uk. 257

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ighaathat-il-Lahfaan (74) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-25-01-1439H-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2017