Mnyama yupi bora kumchinja?


Swali: Ni mnyama upi bora kumchinja katika Udhhiyah; kondoo au ng´ombe?

Jibu: Wanachuoni (Rahimahu Allaah) wametaja kwamba tukichinja mnyama kamilifu basi bora ni ngamia, kisha ng´ombe kisha kondoo na mbuzi. Kondoo ni bora kuliko mbuzi. Ama tukichinja kondoo au mbuzi wasaba na tukalinganisha na ng´ombe mmoja, basi kondoo na mbuzi watakuwa ni bora. Lakini hata hivyo kondoo ni bora kuliko mbuzi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (25/34)
  • Imechapishwa: 20/08/2018