Mnyama wa Udhhiyah mwenye thamani kubwa au mnono?


Swali: Lililo bora katika kichinjwa cha Udhhiyah kiwe ni chenye thamani kubwa  au mnyama mkubwa aliyenona?

Jibu: Mara nyingi ni kwamba ni mambo yenye kulazimiana kwamba mnyama mkubwa aliyenona anakuwa na bei zaidi. Lakini wakati mwingine inakuwa kinyume chake. Tukitazama manufaa ya ule mnyama basi tutasema kuwa kichinjwa kikubwa ndio bora zaidi japokuwa thamani yake itakuwa ndogo. Tukitazama ukweli wa kumwabudu Allaah (´Azza wa Jall) basi tutasema kuwa ambaye ana thamani kubwa ndio bora zaidi. Kwa sababu mtu kutoa pesa nyingi kwa ajili ya kumwabudu Allaah ni dalili inayofahamisha juu ya ukamilifu na ukweli wa ´ibaadah yake. Kwa hivyo jibu tunamwambia mtu huyu atazame kile chenye manufaa zaidi na moyo wake ndio afanye. Midhali kuna manufaa mawili yaliyokutana basi tazama kile chenye manufaa zaidi kwa moyo wako. Ukiona kuwa nafsi inazidi imani yake na kumnyenyekea Allaah (´Azza wa Jall) kwa kumnunua yule mwenye thamani kubwa basi fanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (73) http://binothaimeen.net/content/1677