Swali: Ni sahihi kumchinja mnyama ambaye tumboni mwake ana mimba pamoja na kuzingatia ya kwamba yule ambaye kamchinja alikuwa hajui? Imamu ametoa Khutbah katika swalah ya ´Iyd na amesema kwamba hatoshelezi na hasihi.

Jibu: Kichinjwa ambacho kina mtoto kinasihi. Hili halina shaka. Khatwiyb ambaye amesema kwamba hasihi amekosea. Ng´ombe, ngamia, mbuzi na kondoo ambao tumboni mwao mna mtoto wanasihi na wanatosha pasi na shaka. Ambaye amekhutubu kwamba hawasihi amekosea na amesema maneno ambayo hana hoja yoyote ndani yake. Simjui mwanachuoni yeyote aliyesema hivo. Hilo ni kosa la wazi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/5445/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B6%D8%AD%D9%8A%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AD%D8%A8%D9%84%D9%89
  • Imechapishwa: 15/08/2018