Swali: Kuna mwanamke mjane ambaye mume wake amekufa akamwachia watoto sita wadogo. Vilevile yuko na mtoto mwingine  kutoka kwa mume mwingine. Mtoto huyu ni mwajiriwa na amekwishaoa na ana watoto. Anaishi katika jengo na shangazi na watoto wake wanaishi katika jengo jingine. Lakini hata hivyo wako katika mamlaka moja. Je, inatosha kuchinja mnyama mmoja?

Jibu: Hapana. Kila mmoja anatakiwa kuchinja. Yeye anatakiwa kuchinja kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu wa nyumbani kwake na wale wengine walioko kule wanatakiwa wachinje kwa ajili yao wenyewe. Hapa ni pale ambapo mtu atakuwa na uwezo. Kwa sababu kuchinja ni jambo limependekezwa na sio wajibu. Kukiwepo uwezo basi kila mmoja anatakiwa kuchinja kwa ajili ya nafsi yake, watoto wake na wale walioko katika mamlaka yake. Ni Sunnah mtu kuchinja kwa ajili yake na mke wake, mwanamke na watu wa nyumbani kwake. Yeye anatakiwa kuchinja kwa ajili ya wale walioko katika nyumba yake na nyinyi mchinje kivyenu. Sunnah ni kila mmoja wenu achinje. Kwa sababu mko katika nyumba mbili tofauti.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/11221/%D9%85%D9%86-%D8%A7%D8%AD%D9%83%D8%A7%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B6%D8%AD%D9%8A%D8%A9
  • Imechapishwa: 16/08/2018