Mnafiki?


Swali: Mimi ni kijana ninafunga Jumatatu na Jumanne na ninakuja [Masjid] al-Haram. Lakini hata hivyo nimepewa mtihani wa kuvuta sigara. Je, mimi ni mnafiki?

Jibu: Haya ni maasi. Wewe sio mnafiki, lakini hata hivyo ni mtenda dhambi. Sio kila mtenda dhambi anakuwa mnafiki. Ni juu yako kutubu kwa Allaah na uache kuvuta sigara kwa sababu haina kheri yoyote. Inadhuru. Inadhuru afya, inanuka vibaya na inakera. Sigara haina faida kwa njia hata moja. Ni madhara matupu tu. Tubu kwa Allaah na uachane nayo. Mtake msaada Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13980
  • Imechapishwa: 24/04/2018