Swali: Mtu ambaye analingania katika upotevu na watu wengi hawajui hali yake ambapo tunamuwekea wazi lakini hata hivyo hakomi kuendelea kulingania. Mtu huyu asitiriwe au jambo lake lifichuliwe ili watu watahadhari nae?

Jibu: Ndugu! Anayesitiriwa na kunasihiwa ni yule ambaye dhambi yake imekomeka kwake na wala madhambi yake hayawagusi wengine. Kuhusu yule ambaye madhambi yake yanawagusa wengine kama kwa mfano yuko na madhehebu ya batili au fikira ya kupinda, anawadhuru wengine. Linalotakiwa kwanza anatakiwa kunasihiwa. Akijirudi, himdi zote ni za Allaah, asiporejea akaendelea na wakati huo huo watu ni wenye kudanganyika nae ni lazima kumfichua. Kufanya hivi ni katika kutoa nasaha kwa ajili ya Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake, viongozi wa waislamu na watu wa kawaida.

Kuna tofauti kati ya dhambi ambayo madhara yake yamekomeka kwa mwenye nayo na dhambi ambayo madhara yake hayakomeki kwa mwenye nayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (07) http://alfawzan.af.org.sa/node/2050
  • Imechapishwa: 18/12/2016