Mlinganizi anawatukana watawala wa nchi nyingine

Swali: Khawaarij wameitwa hivo kwa sababu wamefanya uasi dhidi ya mtawala wa waislamu. Inafaa kwa mlinganizi wa Kiislamu wa nchi fulani kumtukana mtawala wa nchi nyingine?

Jibu: Ndio, haya ndio madhehebu ya Khawaarij. Kufanya uasi dhidi ya mtawala kunatofautiana. Kuna kufanya uasi kwa silaha na kufanya uasi kwa maneno. Haijuzu kuchukua fursa ya kutukana na kuponda. Haijuzu kufanya hivo. Kwa sababu jambo hili madhara yake sio kwa mtawala peke yake bali madhara yake ni kwa waislamu kwa sababu ya shari na fitina inayopelekea katika jambo hilo. Mwenye kufanya hivo ametoka nje ya watawala wake na yale waliyomo wanachuoni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=4f8XhuydbZI
  • Imechapishwa: 14/07/2019