Mlinganizi amebarikiwa


Moja katika fadhila za elimu ni kuwa yule mwanachuoni na mlinganizi wameelezwa kuwa ni wenye kubarikiwa. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amembariki. Allaah (Jalla wa ´Alaa) ameeleza kuwa ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا

“Amenijaalia kuwa mwenye ni kubarikiwa popote nitakapokuweko na ameniusia swalah na zakaah madamu niko hai.”[1]

Wasomi wa tafsiri ya Qur-aan wamesema “Amenijaalia kuwa mwenye ni kubarikiwa popote nitakapokuweko” maana yake ni kwamba Unifanye kuwa ni mwenye kuwafunza watu yaliyo na kheri, mwenye kuamrisha mema na kukataza maovu popote nitapokuwa.

وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا

“… na ameniusia swalah na zakaah madamu niko hai.”

Bi maana kutokana na baraka za elimu. Anamuabudu Mola wake (Jalla wa ´Alaa) na sio mwenye kughafilika Naye.

[1] 19:31

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Fadhwl-ul-´Ilm wa Ahlihi wa Swifatuhum http://saleh.af.org.sa/sites/default/files/101.mp3
  • Imechapishwa: 19/03/2017