Mkutano wa mwaka wa Jamaa´at-ut-Tabliygh hauna msingi wowote

Muulizaji: Punde kidogo umetaja kwamba unapendekeza asiwepo yeyote anayesafiri kwenda Pakistan…

Ibn ´Uthaymiyn: Ndio.

Muulizaji: Na umesema kwamba kuna baadhi ya mambo ya ukhurafi…

Ibn ´Uthaymiyn: Ndio.

Swali: Je, uliwahi kuwa katika mikutano hii au ulimtuma mtu mwaminifu huko mpaka uwazungumze?

Jibu: Kuhusu mimi sijawahi kwenda wala sikumtuma yeyote huko. Lakini wale waliosafiri kwenda huko na wakarudi wamegawanyika mafungu mawili. Fungu linasema kwamba huko hakuna kitu kinachopingana na Uislamu. Lakini kile kitendo cha kuwepo mkutano katika wakati maalum na maeneo maalum kwa umati mkubwa wa watu namna hii kana kwamba ni ´iyd inayojirudirudi au kana kwamba ni msimu wa hajj ni jambo lisilokuwa na msingi katika Shari´ah si katika zama za makhaliyfah waongofu wala zile karne zilizokuja baada yao.

Aidha ndugu wengi ambao wanazungumza wanasema kuwa wako na Bid´ah katika mkutano huu. Pengine hawazitaji katika Khutbah, lakini wanachagua viongozi wa baadhi ya makundi na wanawazumgumzia baadhi ya mambo, na khaswa wakiwa si wenye kutoka Saudi Arabia.

Naonelea kwamba muda wa kuwa suala lenyewe haliko wazi na muda wa kuwa msingi wa mkutano huu ambao unakuwa mwaka maalum ni kitu kisichokuwa na msingi katika Sunnah wala katika matendo ya makhaliyfah, kukiacha ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (18 B) Dakika: 16:15
  • Imechapishwa: 10/10/2021