Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

15- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho azungumze [mambo ya] kheri au anyamaze; na yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho amkirimu jirani yake; na yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho amkirimu mgeni wake.”

Kumkirimu mgeni ni kujitahidi kumuonyesha sifa zenye kusifika ambazo huhesabika umemtendea haki [zake]. Sifa zenye kusifika ambazo mgeni huonyeshwa ni kuwa na uso wenye bashasha, furaha, kumkirimu kwa ulimi kwa njia ya kumpokea kwa maneno mazuri na kumlisha. Kumlisha ndio malengo ya Hadiyth hii kwa kuwa ni jambo ambalo wageni huhitajia.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 245
  • Imechapishwa: 14/05/2020