Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

15- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho azungumze [mambo ya] kheri au anyamaze; na yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho amkirimu jirani yake; na yule anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho amkirimu mgeni wake.”

Ni pamoja na kumkirimu jirani kwa maneno mazuri, kumlindia familia yake, heshima yake na nyumba yake. Vilevile kunaingia ndani yake kumhifadhi jirani kwa kutimiza haki nyingine zote za jumla; ukuta ulio kati yao, madirisha yanayoelekea kwake au mahali pa kupaki gari, mahali ambapo watoto wanacheza na mfano wa hayo. Yote haya ni katika kumkirimu jirani.

Vilevile amkirimu jirani kwa chakula, mavazi na mfano wa hayo. Akiwa na chakula amlishe pia jirani yake. ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) alichinja kondoo na akasema:

“Mpelekeeni jirani yetu myahudi.” at-Tirmidhiy (1943)

Hii ni miongoni mwa haki ya jirani ambaye ni kafiri.

Kutokana na hili jopo la wanachuoni – kama Imaam Ahmad na wengine – wanaona kuwa kumkirimu jirani katika Hadiyth hii inahusu jirani ambaye ni muislamu na jirani ambaye ni kafiri.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 241
  • Imechapishwa: 14/05/2020