Mke wangu alinyonya ziwa moja na kaka yangu, ndoa yetu ni halali?

Swali: Nilioa mtoto wa mjomba wangu nikafunga nae ndoa na wala sikumwingilia. Na mke huyu (niliyemuoa) ni dada wa kaka yangu katika kunyonya, yaani alinyonya kwa mamangu na mimi sikunyonya kwa mama yake. Je, ndoa hii ni Halali au Haramu?

Jibu: Ndoa hii haina neno. Maadamu yeye hakunyonya kwa mama yako na wewe hukunyonya kwa mama yake, haina neno. Ama kaka yako kunyonya ziwa moja na mke wako, hili halizingatiwi. Muhimu ni kuwa, hili halina neno ewe muulizaji.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 18/03/2018