Swali: Kuna mwanaume kaoa mwanamke kisha akapotea na hakumpata. Mwanamke huyo akaolewa na ndugu yake mwingine kisha akarejea mume wa kwanza baada ya miaka kumi. Yule wa kwanza na huyu wa pili wote wamezaa nae watoto. Ipi hukumu ya watoto?

Jibu: Ikiwa alimuacha na hakuwa ni mwenye kumpa matumizi au alikuwa ni mwenye kumsubiri huku akitaraji atakuja, yule mwanamke akajivua katika ndoa. Na baada ya kujivua, atakuwa sio Halali kwa yule wa kwanza na atakiwa ni wa huyu wa pili. Ama ikiwa hakujivua, lakini mara nyingi hupeleka mashtaka yake kwa hakimu na kujivua. Na Allaah (Ta´ala) Anasema:

وَلَا تُضَارُّوهُنَّ

“Na wala msiwadhuru.” (65:06)

Akijivua, yule wa kwanza atakuwa hana njia nyingine. Anaweza kujivua ikiwa anadhurika kwa matumizi, maisha na anaogopa kutumbukia katika machafu. Katika hali hii, anaweza kujivua na atakuwa sio Halali kwa yule wa kwanza.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=3083
  • Imechapishwa: 26/02/2018