Mke wa kwanza ana haki ya kuomba makazi yake mwenyewe

Swali: Je inajuzu kwa mke wa kwanza kuomba makazi yake mwenyewe wakati mume wake anapotaka kuoa mke wa pili? Je, kuongeza mke kuna masharti?

Jibu: Swali lako lina mambo mawili:

– Jambo la kwanza, makazi ya yeye mwenyewe kulingana na uwezo wako na kulingana na desturi, hii ni haki ya mke. Na wala haijuzu kwako kumuweka mke wa pili pamoja na mke wa kwanza isipokuwa akiridhia hilo. Akiridhia, ni kama inavyosema mithali:

“Kuridhika ni siri ya hikaya.”

Akikubali kukaa pamoja nae, hakuna neno.

– Jambo la pili, kuongeza mke kuna kanuni. Nayo ni uadilifu katika makazi, kugawiwa siku sawa, matumizi na yanayofuatia hilo. Kila mmoja apewe kiasi cha majukumu alonayo. Nasema haya kwa sababu wanawake wanatofautiana. Mwanamke mwenye watoto kumi na mume, matumizi yake ni makubwa kuliko mwenye watoto watano. Lililo la wajibu ni uwe muadilifu katika hili. Na ikiwa huwezi basi usiongeze mke.

فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً

“… basi oeni waliokupendezeni katika wanawake; wawili au watatu au wanne. Mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi [bakini na] mmoja.” (04:03)

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/4277
  • Imechapishwa: 22/09/2020