Mke mshirikina akisilimu na mume wake akabaki katika dini yake

Swali: Nina dada ambao wameolewa na wanaume washirikina na alipoongoka akataka kuwalingania katika Tawhiyd ambapo dada zake wakaitikia na waume zao hawakuitikia. Je, awatenganishe dada zake kutokamana na waume zao au afanye kitu gani?

Jibu: Wanawake hao wakiwa ni waislamu basi ndoa ni batili. Vilevile ni lazima kuwatenganisha dada zao kutokamana nao na awalazimishe jambo hilo. Kama wako katika nchi ya Kiislamu basi ni lazima kwa mtawala wake kuwatenganisha kutokamana na waume zao makafiri. Ama wanawake hawa wakiwa ni makafiri basi wako sawasawa mfano ni wanawake wa kiyahudi, wanawake wa kikristo au wanawake wenye kuabudu masanamu, basi ndoa yao itakuwa ni sahihi. Wanawake hawa wakisilimu basi itakuwa ni haramu kwao kubaki pamoja nao ilihali wao ni waislamu. Amesema (´Azza wa Jall):

لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

“Wao [wanawake] si halali kwao [makafiri] na wala wao [waume] si halali kwao [hao wanawake].”[1]

Ni lazima kwao kutengana na waume zao makafiri. Isipokuwa tu ikiwa mume atasilimu ndani ya eda. Katika hali hiyo ataendelea kuwa mke wake. Vivyo hivyo baada ya eda kwa mujibu wa maoni sahihi ikiwa mwanamke huyo bado hajaolewa. Basi atamrejea. Ni kama ambavo msichana wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye ni Zaynab (Radhiya Allaahu ´anhaa) alivyorejea kwa mume wake Abul-´Aasw bin ar-Rabiy´ baada ya yeye kuingia katika Uislamu na eda yake ilikuwa imekwisha.

Swalah na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.

[1] 60:10

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (03/141) https://binbaz.org.sa/fatwas/57/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B4%D8%B1%D9%83%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%AA%D8%B2%D9%88%D8%AC%D8%A9-%D8%A7%D8%B0%D8%A7-%D8%A7%D8%B3%D9%84%D9%85%D8%AA-%D9%85%D8%B9-%D8%A8%D9%82%D8%A7%D8%A1-%D8%B2%D9%88%D8%AC%D9%87%D8%A7-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%A7%D9%84%D8%B4%D8%B1%D9%83
  • Imechapishwa: 26/12/2019