Mke kuweka sharti ya kutooa mwanamke mwingine juu yake

Swali: Je inajuzu kwa mwanamke kumuwekea sharti mchumbiaji wakati wa ndoa asioe mke mwingine juu yake pamoja na kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Ameruhusu kuoa wake wane? Ikiwa atamuwekea sharti na mume akakubali hilo, je inawezekana kwa mume baadae akaongeza mke?

Jibu: Masuala haya wanachuoni wametofautiana. Kuna kundi la wanachuoni wameonelea ya kwamba ni wajibu kutimiza hili [ahadi], na kama hakufanya hivyo ndoa inavunjika isipokuwa mpaka kwa ridhaa yake. Haya ndio madhehebu ya wanachuoni wengi.

Kundi lingine la wanachuoni wanaonelea kuwa hii ni sharti isiyokuwepo katika Kitabu cha Allaah, hata kama atakubaliana nae inajuzu baadae kujivua [kwenye kauli yake] na asiitimize. Mimi naegemea katika kauli hii ya mwisho na Allaah ndiye Mwenye kujua zaidi.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/3156
  • Imechapishwa: 21/09/2020