Swali: Kuna mama anamiliki dhahabu na imefikisha Niswaab. Je, inajuzu kuwapa Zakaah dada zake au mume wake ambaye ni mzee na hana mali zaidi ya dhahabu hii anayomiliki?

Jibu: Ndio. Inajuzu kwake kuwapa Zakaah dada zake ikiwa ni mafukara. Na mpaka wa ufukara ni kule kufikia daraja ya kuhitajia ikiwa hawana vya kuwatosheleza. Inajuzu vile vile kumpa mume wake ikiwa ni fakiri. Kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyomwambia Zaynab mke wa ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anha). Alipomuuliza: “Je, ni Halali kwangu kumpa Swadaqah ya mali yangu?” Akasema: “Ndio.”

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1645
  • Imechapishwa: 27/02/2018