Mke kutumia mali ya mume bila yeye kujua


Swali: Je, inajuzu kwa mke kutumia mali yake bila ya mume wake kujua kitu?

Jibu: Hapa wanachuoni wametofautiana. Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa ni sawa akaitumia mali yake ambayo ni maalum kwake hata kama mume wake hakuridhia. Wanachuoni wengine wameonelea kuwa ni lazima mume wake aridhie hilo.

Kwa hali yoyote bora zaidi amtake ushauri mume wake katika hilo kwa ajili ya kuboresha ujumba na kuishi kwa wema.