Mke kupeana mikono na washemeji na kukaa nao faragha

Swali: Inajuzu kwa mwanamke kupeana mikono na ndugu zake na mumewe na kupanda pamoja nao akiwa peke yake kwenye gari?

Jibu: Haifai kwa mwanamke kupeana mikono na kaka, mjomba wala ami ya mumewe. Kwa sababu sio katika Mahram zake. Kwa hiyo haifai kwake akapeana nao mikono, kukaa nao faragha ndani ya gari wala kwengineko. Kwa sababu sio Mahram zake. Mahram zake ni baba yake, babu yake, baba mzaa babu na mfano wa hao. Pamoja vilevile na watoto zake. Ama kuhusu kaka, wajomba na baba wakubwa na baba wadogo wa mume sio Mahaarim. Haifai kwake kupeana mikono na ambao sio Mahram zake. Haifai vilevile akakaa faragha na yeyote; si pamoja na dereva wa kiume wala mtu mwingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3723/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D8%B5%D8%A7%D9%81%D8%AD%D8%A9-%D8%A7%D9%82%D8%A7%D8%B1%D8%A8-%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%88%D8%AC-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%B1%D9%83%D9%88%D8%A8-%D9%85%D8%B9%D9%87%D9%85
  • Imechapishwa: 07/03/2020