Swali: Inafaa kwa mke kumpa zakaah mume wake akiwa ni fakiri?

Jibu: Maoni ya sawa ni kwamba haifai kwa sababu mwanamke huyo anarudi [kwenye usimamizi] kwa mume. Wanachuoni wametofautiana juu ya jambo hili. Lakini maoni ya sawa ni haya niliyosema. Kisa cha Zaynab, ambaye alikuwa ni mke wa Ibn Mas´uud, baadhi wamekifasiri kwamba inahusu zakaah ya faradhi na wengine wamekifasiri kwamba ni zakaah iliyopendekezwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 08/06/2019