Swali: Mwanamke akimtengenezea mume wake vyakula aina mbalimbali, je, kufanya hivi ni katika pumbao la dunia jambo ambalo limekatazwa?

Jibu: Hakuna ubaya kufanya hivi In Shaa Allaah. Na mume ni mtu bora. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحَرِّمُوا طَيِّبَاتِ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكُمْ

“Enyi mlioamini! Msiharamishe vizuri Aliyokuhalalishieni Allaah.” (05:87)

يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ

Enyi bani-Aadam! Chukueni mapambo yenu katika kila Masjid; na kuleni na kunyweni; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu.” (07:31)

Kunapobakia kitu katika chakula, asikimwage bali anatakiwa kukitoa awape masikini na wanaohitaji. Jambo hili ni sahali. Ama mwenye kusema kuwa ni Haramu au haijuzu, haitupasi kwetu kuwaharamishia watu kitu ambacho Allaah Kawahalalishia. Allaah (Ta´ala) Anasema katika Kitabu Chake:

وَلَا تَقُولُوا لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ الْكَذِبَ هَـٰذَا حَلَالٌ وَهَـٰذَا حَرَامٌ لِّتَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ

“Na wala msiseme yanayosifu ndimi zenu uongo; hii halaal na hii haraam ili mumzulie Allaah uongo.” (16:116)

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ

“Ee Nabii! Kwa nini unaharamisha kile Alichokuhalalishia Allaah?” (66:01)

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=555
  • Imechapishwa: 27/02/2018