Swali 729: Inafaa kwa mke kuchukua malipo kutoka kwa mume wake kwa sababu ya kumwandalia chakula wanachokula wote wawili?

Jibu: Ni lazima kwa mwanamke kusimamia yale ambayo yamezoeleka kidesturi za wanawake katika nchi yake kwa kufanya kazi za nyumbani kwake pasi na malipo. Kwa sababu kilichozoeleka kwenye nchi ni kama sharti. Desturi ya nchi yetu iliozoeleka ni kwamba mwanamke anasimamia mambo ya jikoni na mfano wake. Haya ni mambo ya wajibu kwake.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 283
  • Imechapishwa: 08/08/2019