Mke kanilazimisha talaka nikampa kinyume na nia yangu, imepita?


Swali: Kuna mwanamke kaomba Talaka, mume wake akawa amemtaliki kinyume na nia yake. Je, Talaka imepita?

Jibu: Bila ya shaka yoyote. Ikiwa amemtaliki, Talaka imepita. Tumeshatangulia kusema, Talaka ya matamshi ya wazi haishurutishi kutazama nia. Akitamka Talaka ya matamshi ya wazi inapita. Hata ikiwa atasema kuwa: “Mimi nafanya tu mchezo au mzaha, sikukusudia na kadhalika.” Hayakubaliki hayo. Kwa kuwa haya ni matamshi ya wazi. Hakukusudia jengine zaidi ya Talaka. Hakukubaliwi kutoka kwake hoja zingine zaidi ya Talaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/3262
  • Imechapishwa: 27/02/2018