Mke kamlaani mume wake


Swali: Mke wangu alikasirika na akalilaani. Nikamwambia amche Allaah na kwamba hili ni haramu. Ni upi wajibu juu yangu katika hali kama hiyo na nifanye nini ikiwa atakariri laana hizi? Unaninasihi nini.

Jibu: Ni juu yako umnasihi kama ulivyofanya na ukariri nasaha na umkhofishe Allaah. Hili ndilo unalomiliki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/1785
  • Imechapishwa: 20/09/2020