Mke hataki kuvaa Hijaab

Swali: Mume akimuwekea sharti mke ya kuvaa Hijaab ya Kishari´ah na matokeo yake mwanamke akawa amekataa pamoja na hivyo akamnasihi lakini akakataa na jengine ni kwamba hahifadhi swalah – ana haki ya kumtaliki?

Jibu: Ni yeye ndiye mwenye kusimamia talaka kwa hali yoyote ile. Hahitajii kushurutisha chochote. Ikiwa hatengemai amtaliki. Ikiwa haswali, ikiwa havai Hijaab basi amtaliki kwa kuwa anamuasi Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsirayat-12-07-1435-01_0.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2020