Swali: Mke wangu kwa sasa haswali na wala haswali. Na hii ilikuwa ni sharti yangu kwake kabla ya kufunga nae ndoa. Na baada ya ndoa nikawa nimemwacha kwa kiasi cha muda miezi mitano. Ipi hukumu ya Kishari´ah kwa mke kama huyu?

Jibu: Mwanamke asiyeswali hazingatiwi kuwa ni Muislamu, bali anazingatiwa kuwa ni kafiri kutokana na kauli yenye nguvu ya wanachuoni. Kwa kuwa kuacha Swalah ni kufuru kubwa, kwa kuwa Swalah ndio nguzo ya Uislamu. Na imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao (makafiri) ni Swalah, atakayeiacha amekufuru.”

Na hili linawahusu wanaume na wanawake. Na kauli yenye nguvu ni kuwa ni kufuru kubwa, hii ndio kauli sahihi na ndio kauli waliokubaliana Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kama alivyosema ´Abdullaah bin Shaqiyq:

“Maswahabah wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawakuwa wanaona kitu mtu akikiacha ni kufuru isipokuwa kuacha Swalah.”

Hii ni dalili inaonesha kuwa [Maswahabah] (Radhiya Allaahu ´anhum) walikubaliana juu ya hili. Asiyeswali hana kheri yoyote. Ni wajibu kutengana nae kabisa.

لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

“Wao si (wake) halaal kwao (hao makafiri), na wala wao si (waume) halaal kwao.” (60:10)

Na wala usilale nae katika kitanda kimoja, kwani mwanamke huyu hana kheri yoyote, bali ni wajibu kuachana nae.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 19/03/2018