Mke asitumie pesa zake pasina idhini ya mume wake


772- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Si kwa mwanamke kutumia kitu katika pesa zake bila ya idhini ya mume wake.”

Imepokelewa na Tamaam katika “al-Fawaa´id” (2/182/10), at-Twabaraaniy (22/83/201) na Ibn ´Asaakir (4/24) kupitia njia Swahiyh.

Hadiyth ina maanasha ya kwamba haijuzu kwa mwanamke kutumia pesa zake bila ya idhini ya mume wake. Ni katika majukumu kamilifu ya mume na heshima ambayo Mola Wetu (Tabaarak wa Ta´ala) Kawapa wanaume kuhusu wanawake.

Lakini hii haina maana mume atumie hili, ikiwa kweli yeye ni muislamu mwaminifu, hivyo amlazimishe na kumkataza mke kutumia pesa katika mambo yasiyodhuru kitu katika hayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilah al-Ahaadiyth as-Swahiyhah (2/405-406)
  • Imechapishwa: 21/09/2020