Swali: Kuna mtu ameoa mwanamke ambaye anazembea swalah ya Fajr. Mwanamke huyu haswali Fajr isipokuwa pamoja na Dhuhr ilihali mume wake anamuamsha saa moja kabla, lakini hata hivyo haifui dafu. Unamshauri nini Allaah akuhifadhi?[1] Nataraji utamuombea kwa Allaah uongofu.

Jibu: Namuomba Allaah amwongoze na amsaidie mke wake juu yake. Ni wajibu kwake kujaribu kwa kiasi cha uwezo wake amuamshe kwa ajili ya swalah ya Fajr. Vilevile anatakiwa kumwamrisha kulala mapema. Kwa sababu maradhi yaliyowapata watu wengi hii leo kuhusiana na swalah ya Fajr ni kulala wamechelewa. Mwanadamu mwili wake unahitajia usingizi. Tunamuomba Allaah atuongoze.

 [1] Tazama https://firqatunnajia.com/mke-haswali-fajr-ndani-ya-wakati/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49) http://binothaimeen.net/content/1136
  • Imechapishwa: 15/06/2019