Mke anaweza kuomba talaka mume wake akiongeza mke?


Swali: Walii wa mwanamke akimuwekea sharti asioe (mwanamke mwingine) juu ya binti yake, kisha akafanya. Je, ni haki kwa mke kuomba Talaka?

Jibu: Ndio, akimuwekea sharti asioe mwanamke mwingine, sharti ni sahihi kutokana na kauli sahihi ya wanachuoni. Na anaweza kuomba watengane akioa. Na akiendelea kuishi nae, Alhamdulillah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 19/03/2018