Mke anataka kukaa nyumbani kwa kina mume baada ya kufiliwa na mumewe


Swali: Mwanamke huyu amefiliwa na mume wake na anataka kukaa eda siku tatu kwa ajili kuazi nyumbani kwa kina mume pamoja na wanawake wenzie halafu ndio arudi nyumbani kwake ili akamilishe eda.

Jibu: Hapana, haijuzu kufanya hivo. Abaki nyumbani kwake tokea siku ile ya kwanza anapokufa mume. Akae nyumbani kwake mpaka pale atapokamilisha eda. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Baki nyumbani kwako mpaka kitabu kitapofikisha wakati wake.”

Taazia hii haina msingi wowote; watu wanakusanyika siku tatu ni jambo lisilokuwa na msingi wowote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´alaa al-Hawaa´ http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1436-03-02.mp3
  • Imechapishwa: 02/12/2017