Swali: Mimi na mke wangu tuna ugomvi kwa sababu ya utumiaji wa intaneti. Mimi nachelea kwake kwa sababu ya shari na madhara yake ilihali yeye anataka kuitumia kwa sababu ya kuwasiliana na marafiki zake. Anasema kuwa mimi simuamini endapo nitamzuia kuitumia. Unatunasihi nini juu ya hili?

Jibu: Mkataze hilo. Wewe ndiye msimamizi wake na wewe ndiye utakayeulizwa juu yake. Nyumba ni ya kwako. Mkataze hilo. Usiwe mpole kwake juu ya hilo. Mambo haya yanapelekea katika shari na mitihani kwa wanawake na wasichana. Yanapelekea katika shari. Mkataze hilo. Wewe ndiye msimamizi wake.

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ

“Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa vile Allaah amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na pia kwa yale wanayotoa katika mali zao.”[1]

[1] 04:34

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (8) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340429.mp3
  • Imechapishwa: 20/03/2017