Mke anaomba talaka na mume hataki kutoa

Swali: Mke wangu akiniomba talaka mara nyingi ambapo nakataa inahesbaika ni katika dhuluma? Nina dhambi ikiwa nitaiandika kwa siri bila ya mke wangu kujua?

Jibu: Akikuomba talaka kwa sababu humtimizii haki zake au hukumfanyia haki zake na wakati huo huo unamdhulumu, hapa ni lazima umuondolee madhara. Ima uwe mwadilifu au umtaliki:

فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ

“… kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa uzuri.” (02:229)

Ama ikiwa anakuomba talaka bila ya sababu, haijuzu kwake kufanya hivi. Imekuja katika Hadiyth Swahiyh:

“Hakuna mwanamke yeyote anayemuomba mume wake talaka bila ya kuwepo sababu isipokuwa ni haramu kwake harufu ya Peponi.”

 Haya ni matishio makali. Hivyo haijuzu kwake kuomba talaka bila ya kuwepo sababu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13382
  • Imechapishwa: 24/06/2020