Mke anadhikika kwa mume wake kuangalia filamu za ngono

Swali: Mwanamke huyu kutoka Uingereza anasema; nimemvumilia mume wangu miaka sita ambaye anaingia tovuti ya ngono kwenye Intaneti. Ee Shaykh! Unaninasihi nini kwa kuzingatia ya kwamba sijamwambia yeyote zaidi yako wewe. Ardhi imenikuia dhiki na jambo hili kwangu limekuwa zito na siwezi kumkabili mume wangu binafsi. Unaninasihi nini? Je, nende kwa familia yangu au nimnasihi na kuzungumza naye? Ninaapa kwa Allaah ya kwamba niko katika dhiki isiyojua yeyote zaidi ya Allaah.

Jibu: Allaah akubariki. Kitendo chako hichi kinajulisha kheri na himdi zote ni za Allaah. Vilevile kinajulisha ghera [yako ya dini]. Lakini pamoja na hivyo mnasihi ukiwa wewe na yeye tu. Mnasihi na ukariri nasaha. Akikubali, ni vizuri, asipokubali na kile kitendo chako cha wewe kwenda kwa familia yako kikiwa kina taathira kwake na kitamfanya yeye kuachana na jambo hili, nenda kwa familia yako kwa sababu hii ni sababu inayosikizika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2138
  • Imechapishwa: 12/07/2020