Mke anachukua pesa kutoka kwa mume wake

Swali: Inajuzu kwa mke kuchukua pesa kutoka kwa mume bila ya mume wake kujua pamoja na kuzingatia ya kwamba anamjali na anampa mahitajio yake yote? 1.15

Jibu: Hapana. Ikiwa anamsimamia matumizi ya wajibu, basi asichukue chochote pasi na idhini yake. Ama ikiwa anapunguza kitu katika matumizi na hampi wakati anapomuomba, achukue kiwango tu kile kinachomtesheleza. Hind bint ´Utbah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alisema:

“Ee Mtume wa Allaah! Abu Sufyaan ni mwanaume bakhili. Ni dhambi nikuchukua mali yake kwa ajili ya kulisha familia yetu?” Akamwambia: “Hapana, chukua kinachokutosheleza kwa wema.”[1]

Ikiwa mtu hapati haki yake kutoka kwa mtu anayeipinga au anayechelewesha kulipa deni, achukue haki yake.

[1] Muslim (1714).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (63) http://alfawzan.af.org.sa/node/16495
  • Imechapishwa: 26/08/2017