Swali 40: Ni ipi hukumu kwa ambaye anakuwa mbali na mke wake miaka mitano au kumi? Je, mke ana haki ya kumuomba talaka au kufutwa kwa ndoa?

Jibu: Mwanamke akidhurika japokuwa ni kwa mwezi mmoja, miezi mitatu au miezi mine ambapo akaenda na asimwachie matumizi, makazi na akamtelekeza kwenye nyumba na asiweze kukaa ndani yake peke yake basi ana haki ya kuomba ndoa ifutwe. Aende kwa hakimu au Qaadhiy katika nchi yake na aombe ndoa ifutwe. Ana haki ya kufanya hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 75
  • Imechapishwa: 27/12/2019