Swali 807: Vipi ikiwa mwanamke na familia yake wakiweka sharti asitolewe nje ya nyumba yake wala mji wake?

Jibu: Mwanamke au walii wake akimuwekea sharti mwanaume kubaki katika mji wake na kutohama pamoja na mume wake kwenda mji mwingine ni sharti sahihi ambayo ni lazima kuitendea kazi. ´Uqbah bin ´Aamir amepokea ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Masharti ambayo ni wajibu zaidi kwenu kuyatimiza ni yale mliyofanyiwa halali kwa tupu zenu.”

al-Athram amepokea kwamba kuna mwanaume alimuoa mwanamke ambaye alimuwekea sharti ya kulazimiana na nyumba yake ambapo baadaye mwanaume akataka kumuhamisha. Wakaenda kwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) hali ya kuwa ni wenye kugombana ambapo akasema: “Ana haki ya kulazimiana na sharti yake. Lakini mke akitaka kuhama pamoja naye, ana haki ya kufanya hivo, na akitaka kuidondosha imedondoka.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 319
  • Imechapishwa: 04/08/2019