Mkate na pesa katika Zakaat-ul-Fitwr


585- Nilimsikia Ahmad akiulizwa kama inafaa kutoa mkate katika Zakaat-ul-Fitwr. Jibu lake lilikuwa:

“Hapana.”

Nilikuweko na nikisikiliza wakati ambapo Ahmad aliulizwa kama inafaa kutoa pesa katika Zakaat-ul-Fitr. Akajibu:

“Nakhofia kutosihi. Ni jambo linakwenda kinyume na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 123
  • Imechapishwa: 05/03/2021