Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema kwamba yeye anajua yaliyofungamana na manufaa ya Da´wah zaidi kuliko Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Manen haya ni batili na kufuru. Huku ni kumtia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika ujinga. Hili linaingia katika lile fungu la kwanza la maneno ya Shaykh:

“Mwenye kuamini kwamba uongofu wa mwingine asiyekuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mkamilifu zaidi kuliko uongofu wake ni kafiri.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 110
  • Imechapishwa: 17/11/2018