Swali: Ikiwa katika nchi ya kikafiri kuna mji ambao unajulikana kuwa na Ahl-us-Sunnah wengi na wamekusanyikana katika mji huo. Je, mji huu unakuwa mji wa kufanyia Hijrah (Daar-ul-Hijrah) kwa haki ya yule ambaye hakuweza kufanya Hijrah katika nchi miongoni mwa nchi za Kiislamu?

Jibu: Hapana, hauzingatiwi kuwa ni mji wa kufanyia Hijrah. Kinachozingatiwa ni kiongozi. Ikiwa mji huo kiongozi wake ni Muislamu, unazingatiwa kuwa ni mji wa Kiislamu hata kama ndani yake kutakuwa makafiri. Ama ikiwa kiongozi ni kafiri, haijalishi kitu hata kama Waislamu ndio watakuwa wakazi wake wengi, hauzingatiwi kuwa ni mji wa Kiislamu.

Lakini hata hivyo ni mwenye kupewa udhuru ikiwa hajaweza kufanya Hijrah. Aishi katika nchi ya kikafiri kiasi cha udhuru tu.

[Vilevile] unakuwa ni mji wa Kiislamu ikiwa kiongozi anahukumu kwa Shari´ah. Huu ndio mji wa Kiislamu. Ama ikiwa anahukumu kinyume na Shari´ah, huu ni mji wa kikafiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (58) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-01-14.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020