Mji mzima una msikiti mmoja wenye kaburi

Swali: Msikiti ulio katika mji wetu una kaburi na hatuna msikiti mwingine usiokuwa huo. Je, inajuzu kwangu kuswali ndani yake?

Jibu: Hapana. Usiswali ndani yake. Jengeni msikiti katika mji wetu na mswali ndani yake. Hata kama hamkujaaliwa kujenga kwa mfano inaweza kuwa kiwanja cha wazi mkakiandaa na mkaswali hapo mpaka pale mtapojaaliwa kujenga msikiti usiokuwa na kaburi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (87) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd-3-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 10/11/2018