Mjane hataki kuolewa tena baada ya mume wake kufariki

Swali: Imeruhusiwa kwa mwanamke kijana kukataa kuolewa baada ya kufiliwa na mume wake wa kwanza?

Jibu: Shari´ah imesisitiza kuoa/kuolewa na ikakokoteza kwalo. Ni wajibu kwa msimamizi wa mwanamke huyu amsihi kuolewa na amsisitize. Akikataa na wakati huohuo kukawa hakukhofiwi juu yake fitina amwache na jambo lake.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (18/30)
  • Imechapishwa: 20/08/2017